Wednesday, July 15, 2020

MAJALIWA ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA TENA UBUNGE WA RUANGWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkewe Mary Majaliwa wakikaribishwa na Katibu wa CCM wa Wilaya  ya Ruangwa, Barnabas Essau (kulia) wakati walipowasili kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo kuchukua fomu za kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, Julai 15, 2020. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa  fomu za kuwania tena ubunge wa jimbo la Ruangwa na Katibu wa CCM wa wilaya  ya Ruangwa, Barnabas Essau kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, Julai 15, 2020. Kushoto ni mkewe Mary Majaliwa.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha fomu za kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa baada ya kuzichukua, kuzijaza na kuzirejesha, Julai 15, 2020. Kushoto ni Mkewe Mary Majaliwa. 

Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kurejesha fomu za kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa, Julai 15, 2020. Kulia ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Barnabas Essau. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirejesha fomu za kugombea tena ubunge wa Jimbo la Ruangwa kwenye ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa baada ya kuzichukua na kuzijaza,kushoto ni Mkewe Mary Majaliwa, Julai 15, 2020.

Read More

Monday, July 13, 2020

WAZEE NACHINGWEA WAMCHANGIA RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU AWASHUKURU AAHIDI KUFIKISHA SALAMU.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mzee Hamis Kambona (wapili kutoka kushoto) wakati akipokea  mchango wa Shilingi laki moja kutoka kwa wazee wa wilaya na Nachingwea kwa ajili ya kumchangia, Rais Dkt.  John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa  mwaka huu, kwa kutambua mchango mkubwa katika kuiletea Tanzania maendeleo. Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea wakati Waziri Mkuu alipowasili akiwa jiani kwenda Ruangwa, Julai 13, 2020. 


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipokea risiti ya malipo ya shilingi Laki moja kutoka kwa Mzee Abdalah  Saidi Kaliondima, kwa ajili ya kumchangia, Rais Dkt. John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, kwa kutambua mchango mkubwa katika kuiletea Tanzania maendeleo, Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea wakati Waziri Mkuu alipowasili akiwa jiani kwenda Ruangwa, Julai 13, 2020. 

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwashukuru wazee wa wilaya na Nachingwea baada ya kupokea risiti ya malipo ya shilingi Laki moja walizozitoa kwa ajili ya kumchangia, Rais Dkt.  John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa  mwaka huu, kwa kutambua mchango mkubwa katika kuiletea Tanzania maendeleo. Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea wakati Waziri Mkuu alipowasili akiwa jiani kwenda Ruangwa, Julai 13, 2020.

Read More