Wednesday, November 6, 2019

MAJALIWA ASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA KAKA YAKE MZEE BAKARI MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika mazishi ya marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa , Novemba 6, 2019. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Venance Mabeyo na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya  Usalama wa Taifa, Diwani Athumani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Mke wa Waziri mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwa na Kamishina Jenerali wa Uhamiaji , Dkt, Anna Makakala (katikati) na katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge (kushoto) katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirika katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Venance Mabeyo (kushoto), Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani (kulia) baada ya wote kushiriki katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika sala ya kumwombea marehemu kaka yake, Mzee Bakari Majaliwa iliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. Wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon Siro katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika  katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee, Bakari Majaliwa yaliyofanyika  katika kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala katika mazishi ya kaka yake Waziri Mkuu, Mzee Bakari Majaliwa yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Novemba 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read More

MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA MWANASIASA MKONGWE WILAYANI RUANGWA MZEE MMUYA

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamanı wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Kaspar Selemani Mmuya katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nangumbu kwenye kitongoji cha Mtakuja wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitupa udongo kwenye kaburi la mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamanı wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Kaspar Selemani Mmuya katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nangumbu kwenye kitongoji cha Mtakuja  wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa zamanı wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Kaspar Selemani Mmuya katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Nangumbu kwenye kitongoji cha Mtakuja wilayani Ruangwa, Novemba 5, 2019.

Read More

Tuesday, November 5, 2019

MATUKIO YA MHESHIMIWA WAZIRI MKUU BUNGENI 5.11.2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa Tablets na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai wakati la ugawaji wa tablets kwa Wabunge wote, katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Wabunge, wakati akiingia Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Salma Kikwete, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read More