Thursday, February 7, 2019

WAZIRI MKUU,KASSIM MAJALIWA AKIJIBU MASWALI YA PAPO KWA HAPO BUNGENI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka  Mbunge wa Mchinga, Hamidu Hassan Bobali ambaye aliuliza swali katika kipindi  cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uwekezaji , Angela Kairuki baada ya kujibu vizuri sana maswali ya papo kwa papo, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Read More

TFF HAKIKISHENI TUNAIBUKA NA USHINDI AFCON-MAJALIWA

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lihakikishe Tanzania inaibuka na ushindi katika fainali za michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 barani Afrika (AFCON) yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini Tanzania.

Ametoa agizo hilo leo asubuhi (Alhamisi, Februari 7, 2019) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge waKilolo, Venance Mwamoto.

Mbunge huyo alitaka kufahamu Serikali imeyahusishaje mashindano hayo ya AFCON na mkakati wa kuendeleza utalii nchini, ambapo Waziri Mkuu amesema maandalizi yote yanaendelea kufanyika na Serikali imejiandaa vya kutosha kupokea wageni hao.

Waziri Mkuu amesema TFF inaendelea na maandalizi ya mashindano hayo ya vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kuipa Tanzania uenyeji wa fainali hizo.

Amesema Watanzania wanatakiwa wawe wazalendo na kuipa ushirikiano timu yao ili kuhakikisha inaibuka mshindi kwenye fainali hizo.

Pia Waziri Mkuu amesemaWizara ya Maliasili na Utalii itatumia mashindano hayo kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.“Tutawapeleka Kilwa wakaone majengo ya zamani yaliyokaliwa na Waarabu na maeneo mengine.”
Waziri Mkuu amewasihi Watanzania kutumia fursa ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika nchini kwa kufanya shughuli mbalimbali zitakazowaongezea kipato.“Kwa kupitia mashindano hayo sisi kama Watanzania tumejipanga huduma zote zipo , za Chakula, Hoteli na usafiri.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Wizara Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kazi kubwa ya kushawishi  FIFA kuyaleta mashindano haya hapa nchini pamoja na ujio wa Rais wa FIFA, pia TFF kwa uratibu wa mashindano hayo sasa.



(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma,                       
ALHAMISI, FEBRUARI 7, 2019
Read More

MAJALIWA BUNGENI LEO TAREHE 07.02.2019

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.  Phillip Mpango, bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Kilosa mkoani Morogoro kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Monica ya Arusha kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Kushoto kwake ni Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso na kulia kwa Waziri Mkuu ni  Mwalimu Mkuu  wa shule Msaidizi, Sista Colletah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi  ya Assumption ya Arusha, Ritta Deo Moshi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Mtoto huyo na wenzake walikwenda bungeni kujifunza shughuli mbalimbali za Bunge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi  ya Assumption ya Arusha, Ritta Deo Moshi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Mtoto huyo na wenzake walikwenda bungeni kujifunza shughuli mbalimbali za Bunge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Read More

Tuesday, February 5, 2019

TUMIENI IPASAVYO WIKI YA SHERIA-MAJALIWA

Asema uelewa mdogo wa sheria unachangia wananchi kupoteza haki

MASUALA ya kisheria si mepesi kujulikana kwa kila mwananchi na kwa sababu hiyo, wananchi wengi wamekuwa na uelewa mdogo wa masuala hayo, jambo linalochangia baadhi kukosa au kupoteza haki zao. 

Pia, wananchi wengi hawajui taratibu na mienendo ya kimahakama, hivyo wamekuwa wakipoteza haki kwa kigezo cha kutofuata taratibu ili kupata haki zao hizo na wakati mwingine unaweza kukuta ni suala dogo tu.

Kila mwaka, Mahakama ya Tanzania imekuwa ikiadhimisha Wiki ya Sheria, ambapo pamoja na mambo mengine, wiki hiyo imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi kwa kuwa inatoa fursa ya wananchi kupata elimu kuhusu masuala ya sheria.

Maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria yamekuwa yakifanyika kimkoa na kitaifa kwa wadau mbalimbali wa masuala ya sheria kutoa huduma kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kusikiliza masuala yao na kuyapatia ufumbuzi na kwa yale ambayo huhitaji ufumbuzi zaidi, hupewa msaada.

Kwa mwaka huu, maadhimisho ya Wiki ya Sheria, yamefanyika kwa mara ya kwanza Jijini Dodoma, baada ya Serikali kuhamishia makao makuu ya nchi katika jiji hilo.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo wadau wa sheria. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Akifungua maadhimisho hayo, Waziri Mkuu aliwataka wananchi wayatumie ipasavyo maadhimisho hayo ili waweze kupata elimu na huduma mbalimbali za kisheria.

Majaliwa alisema wananchi wa mikoa mbalimbali, ukiwemo Dodoma, wanatakiwa kutumia maadhimisho hayo kwa kujitokeza kwa wingi kupata elimu na kwa wale wenye matatizo ya kisheria kuyaeleza ili yatatuliwe.

“Kwa yule ambaye hana tatizo, aje kupata elimu ya sheria, kutoa maoni au mapendekezo yake kuhusu mfumo mzima wa utoaji wa haki. Waswahili husema, elimu haina mwisho. Kwa kuwa elimu ya sheria imesogezwa hapa Dodoma, tumieni fursa hii kujifunza kadri iwezekanavyo,” alisema.

Waziri Mkuu alibainisha kuwa, Serikali imeendelea kushirikiana na mhimili wa Mahakama katika kuhakikisha huduma bora za utoaji haki zinawafikia wananchi kwenye maeneo wanayoishi kwa wakati.
“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ni mdau muhimu wa Mahakama na inafuatilia kwa karibu changamoto zote zinazoikabili pamoja na wadau wengine katika mfumo wa utoaji haki,” alibainisha. 

Waziri Mkuu alisema  dhamira ya Mahakama kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), katika kuleta mabadiliko ya utoaji haki ni hatua nzuri na itasaidia kuboresha utoaji wa haki kwa wakati.

Hivyo, Waziri Mkuu aliwasihi watumishi wa Mahakama kujikita katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA bila kukatishwa tamaa na changamoto zitakazojitokeza kwani mara nyingi kitu kipya chochote hakikosi changamoto za hapa na pale. 

“Binafsi naunga mkono uamuzi wa Mahakama kutumia TEHAMA katika usajili wa mashauri, kwani unakwenda sanjari na azma ya Serikali kuhakikisha TEHAMA inatumika vema kwenye taasisi za umma,” alisema.

Aliongeza kuwa matumizi ya TEHAMA katika taasisi za umma yanalenga kutoa huduma bora na kuipunguzia Serikali na mihimili mingine gharama za uendeshaji, hususan katika utoaji huduma kwa wananchi.

Alisema lengo la Serikali ni kuona huduma bora zinawafikia wananchi kwa urahisi na pia zinapatikana kwa wakati.

“Nitoe wito kwa wadau, wakiwemo mawakili wa serikali na wa kujitegemea, kutumia mifumo hiyo katika kusajili mashauri na wasiwe wao wa kwanza katika kulaumu na kubeza,” alisema. 

Waziri Mkuu alisema mawakili wote wa Serikali na wa kujitegemea, wanapaswa kuwa sehemu ya kutatua changamoto zitakazoibuka katika matumizi ya mifumo hiyo kwa kuwasilisha mapendekezo kuhusu namna bora ya kuiboresha. 

Alisema  matumizi ya TEHAMA si tu yatawawezesha kutoa huduma kwa wakati, bali pia  yataweka uwazi, ambao utawapunguzia malalamiko mengi kuhusu watumishi na utoaji haki. 

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa  Wiki ya Sheria ni muhimu kwa mfumo mzima wa utoaji haki nchini. “Endeleeni kuienzi na itumieni vizuri katika kufanikisha malengo ya Mahakama ya kumpatia haki kila mwananchi bila ubaguzi.” 

Kwa upande wake, Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma, alisema  kwa kipindi cha wiki nzima, maonyesho ya Wiki ya Sheria yatafanyika Jijini Dodoma  na kwenye Mahakama zote nchini, kuanzia ngazi ya wilaya.

Profesa Juma alisema  kupitia maonyesho hayo, wananchi watakaoshiriki na kutembelea mabanda, watapata elimu na kutathmini umuhimu na hadhi ya mfumo wa kimahakama katika kustawisha maisha yao pamoja na kuwasaidia kupata haki kwa mujibu wa sheria.

“Kujikumbusha umuhimu wa Mahakama kutoa haki kwa wakati, kuzingatia misingi ya maadili na Mahakama kuendeleza programu za maboresho yanayolenga kupeleka huduma za utoaji haki karibu zaidi na wananchi,” alisisitiza.

Jaji Mkuu aliwakumbusha viongozi wa vijiji, kata, wilaya, mkoa, idara na wizara, wabunge, majaji, mahakimu na watumishi wa umma, wahudhurie maonyesho hayo ya Wiki ya Sheria bila kukosa.

Alitolea mfano banda la maonyesho la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwamba, kwa wale watakaoshiriki, watakumbushwa  kuwa mamlaka ya mihimili mitatu ya dola yanatokana na nguvu ya sheria, ambayo haimuonei mwananchi yeyote.

Katika maadhimisho hayo, ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika nje ya Jiji la Dar es Salaam, Waziri Mkuu alishiriki matembezi ya kilomita tano akiwa na Jaji Mkuu, Profesa Juma na viongozi wengine, yakianzia Mahakama Kuu Dodoma hadi viwanja vya Nyerere Square na kisha alitembelea mabanda.


 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma,                       

JUMANNE, FEBRUARI 5, 2019.
Attachments area
Read More

Saturday, February 2, 2019

MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuadhimisha Wiki ya Sheria, jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya mazoezi ya viungo nje ya viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019, baada matembezi ya kuadhimisha Wiki ya Sheria, kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya mazoezi ya viungo nje ya viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019, baada matembezi ya kuadhimisha Wiki ya Sheria, kutoka kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mifumo ya kisasa ya Mahakama Mtandao wakati alipokagua mabanda katika kuadhimisha Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019 kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tehama Kalege Anock, Athumani Kanyegezi na Jaji Mkuu wa Tanzania Ibrahim Juma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Fatma Karume, wakati alipotembelea mabanda katika Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019.
Wananchi waliyohudhuria katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi waliyohudhuria katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria, iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijjini Dodoma  Februari 2, 2019.
Read More