Saturday, August 11, 2018

NAMUNGO FC KUPAMBANA NA SIMBA YA JIJINI DSM


*Ni katika uzinduzi wa uwanja wa Halmashauri ya Ruangwa

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ruangwa kesho (Jumamosi, Agosti, 11, 2018) inatarajia kuzindua uwanja wake wa michezo, ambapo timu ya wilaya hiyo Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza itapambana na bingwa wa ligi kuu 2018/2019 Simba SC ya jiji Dar es Salaam.

Timu hiyo ya Namungo FC ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini, imeupa heshima mkoa wa Lindi kwa kuwa ndiyo pekee inayoshiriki ligi daraja la kwanza. 
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa uwanja huo leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mbali na timu ya Simba pia timu hiyo inatarajia kucheza na timu za Yanga , Azam za jijini Dar es Salaam na Dodoma FC ya jijini Dodoma.
Uwanja wa mpira wa miguu wa wilaya Ruangwa unaoitwa Majaliwa Stadium umejengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndio utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo FC kuchezea mechi za nyumbani.  
 “Lazima tuisapoti timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”
Kadhalika Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa timu ya Namungo FC kucheza na timu kama za Simba, Yanga, Azam na Dodoma FC kwa sababu zinasaidia katika kuimarisha viwango vya wachezaji na kuwaondolea uoga wa kupambana na timu nyingine.
Kiingilio katika mechi ya Namungo FC na Simba SC ni sh. 3000. Tayari timu ya Simba imeshawasili wilayani Ruangwa leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018), saa 11.01 jioni kwa ajili ya mechi yake na timu ya Namungo.
Read More

UWANJANI RUANGWA LEO 11.08.2018

Mashabiki wa soka, wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Simba SC na Namungo FC kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Agosti 11.2018 .

Mashabiki wa soka, wakiwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya Simba SC na Namungo FC kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Agosti 11.2018 .

Read More

Friday, August 10, 2018

ZIARA YA WAZIRI MKUU RUANGWA

Wananchi wa kijiji cha Likunja wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliposimama na kuzungumza nao, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Likunja Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 10.2018 

Wananchi wa kijiji cha Likunja wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliposimama na kuzungumza nao, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua uwanja wa mpira wa Kassim Majaliwa Stadium Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 10.2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na wachezaji wa Namungo FC, alipowatembelea kambini kwao Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akionesha jezi ya Namungo FC, baada ya kupokea jezi hizo zilizotolewa na wafadhili wa timu hiyo, Haojue Company Limited Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 Kushoto ni Mkurugenzi wa Haojue Brand Martin Francis.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea kiatu kwa naiba ya Namungo FC, kutoka kwa Mkurugenzi wa Haojue Brand Martin Francis, Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018

Read More

Thursday, August 9, 2018

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KATA YA MNACHO-RUANGWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo katika Kijiji cha Chimbila B, Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku nne, Agosti 9 2018

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua darasa la kompyuta katika Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018, kulia ni Kaimu Mkuu wa Shule Muhsin Ibrahim.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Kaimu Mkuu wa Shule Muhsin Ibrahim, baada ya kukagua darasa la kompyuta katika Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa Agosti 9 2018. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018. 

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018.


Wananchi wa Kata ya Mnacho wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akiwahutubia kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Mnacho, Wilayani Ruangwa, Agosti 9 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chimbila B, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Mnacho iliyopo kwenye Kata ya Mnacho, Agosti 9 2018. 

Read More

Wednesday, August 8, 2018

VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wabadilike na watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kulalamika.

Amesema kama kuna changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasilina na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Agosti 8, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Nandagala.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa, alisema vijana wanatakiwa kujitambua na kuiunga mkono Serikali kwa kufanyakazi kwa bidii.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa pamoja katika kubuni shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo litawakwamua kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama.
PiaWaziri Mkuu aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Read More

MAJALIWA AKIWA RUANGWA

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa kata ya Nandagala wakati akiwasili katika uwanja wa zahanati ya kijiji cha Nandagala kwa jailli ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Agosti 8.2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani humo, Agosti 8.2018 .

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimshuhudia aliyekua Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018 

Aliyekua Mwenyekiti wa Kata ya Nandagala Jafari Omari (katikati), akikabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Agosti 8.2018 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Nandagala Wilayani Ruangwa,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Nandagala Wilayani Ruangwa,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018

Read More