Thursday, June 28, 2018

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI - JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 9 18, 2018



Read More

Wednesday, June 27, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA, DKT. DAU


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Dau, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma Juni 27, 2018.


Read More

MAJALIWA AZINDUA VITUO 51 VYA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA WILAYNI BAHI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe wakati alipozindua vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.  Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika  uzinduzi wa vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.   Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. Wanne kushoto ni Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie Boucly.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chombo cha kupima wingi wa mvua baada ya kuzindua vituo 51 vya kufuatilia  taarifa za hali ya hewa katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Juni 27, 2018.  Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama,Waziri wa Maji, Mhandisi Isaack Kamwele, Mwakilishi Mkaazi wa Mpango  wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bibi Natalie  Boucly na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoa wa Dodoma, Felista Bura

Read More

Monday, June 18, 2018

TANZANIA INAONGOZA KWA UCHUMI KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema taarifa ya Kongamano la Uchumi la Dunia la mwaka 2018 inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na uchumi jumuishi miongoni mwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Amesema hali hiyo, imetokana na Tanzania kufungua fursa za ujasiriamali ambapo kuna zaidi ya biashara milioni tatu zinazokuwepo kila mwaka, lengo la nchi ni kuhakikisha kuwa uchumi unakua na unamgusa kila Mtanzania hususan mwananchi wa kawaida.

Waziri Mkuu ameyasena hayo leo (Jumatatu, Juni 18, 2018) wakati akifunguaKongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa LAPF, jijini dodoma.

“Pia, huduma za fedha jumuishi ni kigezo ambacho kimeiweka Tanzania mahala pazuri kwenye uchumi jumuishi ambapo zaidi ya Watanzania milioni 30 wamekuwa wakifanya miamala mbalimbali ya fedha kupitia simu za mkononi na hivyo kuongeza huduma za fedha kufikia asilimia 65,” amesema. 

Amesema huduma za msingi za kijamii kama vile elimu, afya na kupungua kwa rushwa katika utoaji huduma za umma pamoja namtandao wa miundombinu ya barabara ambayo huwezesha wananchi wengi kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ni kigezo kingine kilichozingatiwa katika kuipatia Tanzania nafasi hiyo. 

Waziri Mkuu ameongeza kwamba Serikali inaamini kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa kasi kubwa na matokeo yake yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, soko la huduma na shughuli nyingine za kiuchumi. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema suala la uchumi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ni moja ya ajenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo amezitaka sekta zote zihakikishe zinatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa viwanda.

Pia amesema suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi lazima liende sambamba na uwezeshaji vijana kujiajiri kama inavyoelekeza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015. “Ilani inatambua kwamba kuwawezesha wananchi kiuchumi ni hatua ya msingi katika kujenga Taifa lililoimarika kiuchumi na lenye lengo la kujitegemea,”. 

Aidha, Ilani pia, inasisitiza kuhusu umuhimu wa kuhamasisha ushiriki wa Sekta binafsi katika kuwezesha wananchi kiuchumi, hivyo ni muhimu kukamilisha taarifa ya uwezeshaji kutoka kwa wadau wa sekta binafsi, ili Serikali iweze kuona mchango wa sekta binafsi katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa malengo hayo ya uwezeshaji wananchi katika maeneo ya fursa za mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ya masharti nafuu ni muhimu sana katika kupambana na umaskini wa kipato. 
         
Amesema kwa kutambua umuhimu wa ajenda ya uchumi wa viwanda, ndiyo maana makongamano ya uwezeshaji yamekuwa yakiweka mkazo kwenye masuala ya viwanda. Hali hiyo pia, inajidhihirisha katika kaulimbiu ya Kongamano la Tatu ambayo ni: “Viwanda: Nguzo ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi”. 

Hivyo Waziri Mkuu ameongeza kwa kusema, “tuendelee kuhimiza kuhusu kutekeleza uchumi wa viwanda kwa lengo la kuwawezesha wananchi wetu kiuchumi na kuhakikisha kuwa tunafikia lengo la kuwa na  uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,”.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba, Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Bw. Suleiman Jafo.

Wengine ni Wakuu wa Mikoa mbalimbali, Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, Makatibu Tawala wa Mikoa, Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,Wakurugenzi wa Halmashauri za Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng’ Issa, wadhamini wa Kongamano hilo na Wawakilishi kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta binafsi.
Read More

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI - JIJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 9 18, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Jinana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.

Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakipiga makaofi baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, Faustine Kamuzora, Meya wa jiji la Dodoma,Profesa Davis Mwamfupe, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada ya kuizindua  katika Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada ya kuizindua  katika Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mhandisi, Salome Kabunda  kutoka TANROADS  Tuzo ya Uwezeshaji Kiuchumi, baada ya TANROADS kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara, Wakala na Idara za Serikali kwenye  Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofunguliwa na Waziri Mkuu katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.


Read More

Saturday, June 9, 2018

WATUMISHI WA OFISI WAZIRI MKUU WAPEWA MAFUNZO YA KUZIMA MOTO



Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Joseph Mboje akizima moto kwa kutumia kifaa rasmi cha kuzima moto katika mafunzo ya kuzima moto yaliyoendeshwa na Maofisa wa Kikosi cha Zimamoto cha jijini Dodoma Mei 12, 2018. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Ruth Mwasakafyuka akizima moto katika mafunzo  ya kuzima moto kwa kutumia kifaa rasmi cha kuzima moto yaliyoendeshwa na Maofisa wa Kikosi cha Zimamoto cha jijini  Dodoma Mei  12, 2018. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Read More

MAJALIWA AKUTANA NA ASKOFU MKUU WA EAGT DKT. MWAKIPESILE



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt. Brown Mwakipesile, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 12, 2018.
Read More

Friday, June 1, 2018

ZIARA YA MAJALIWA RUANGWA



  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary  Majaliwa  (wapilinkulia)  akitoa msaada wa shuka na mito kwa wazazi wote waliojifungua na waliokuwa wakisubiri kujifungua kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya wilaya ya Ruangwa  Aprili 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea soko kuu la wilaya ya Ruangwa kakagua hali ya upatikanaji na bei za vyakula akiwa katika jimbo lake la uchaguzi Aprili 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)



 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary wakikabidhi baiskeli kwa walemavu Kanisia  Ndaka (wapili kulia na na Rehema Mtachi (wapili kushoto)  kwenye uwanja wa michezo wa mjini Ruangwa Aprili 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Read More